Safari za usiku zapunguza vurugu msimu wa sikukuu.
–Na Admin Wetu
UPATIKANAJI wa usafiri wa mabasi kuelekea mikoa mbalimbali nchini saa 24 nyakati za asubuhi, mchana na usiku kumetajwa kuwa chanzo cha kupungua kwa adha ya usafiri kuelekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Walisema pia ukataji wa tiketi mtandaoni umechangia kutopanda kwa nauli huku wengine wakidai kuwa upandishaji wa nauli hutokana na tamaa za wamiliki wa vyombo vya usafiri.
Mohamed Juma alilieleza HabariLEO kuwa matumizi ya tiketi za mtandaoni na kuwepo kwa usafiri kwa saa asubuhi, mchana na usiku imerahisisha upatikanaji wa usafiri huo.
“Msimu huu nauli zimebaki palepale bado tunatumia nauli zilezile za mwaka jana. Lakini watakaoamua kupandisha nauli, wachukuliwe hatua,’’ alisisitiza.
Naye, Mwanaisha Salum alisema kuwa miaka iliyopita kulikuwa na shida ya usafiri pamoja na kupanda kwa nauli kutokana na idadi kubwa ya wasafiri, lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti.
“Nimesafiri usiku kwa basi kutoka Dar es Salaam kuja hapa Mbeya, kwenye basi kulikuwa na nafasi saba hazina watu, pia nauli ni ile ile ya Latra, nimeshangaa sana kwani sijazoea kuona hali hii mwishoni mwa mwaka. Nadhani hali ya uchumi imechangia watu wengi kutosafiri mwaka huu,” alisema Salum.
Hatua ya mabasi kusafiri saa 24 imesaidia kupunguza msongamano wa abiria ambao ulikuwa ukiendelea hasa mwishoni mwa mwaka.
-Admin...
There are 3 comments
John Sanweli December 16, 2024 at 4:39 pm
Reply Wamiliki wa mabasi kutoa tiketi za kieletroniki ili kuondoa ukwepaji wa kodi kwani baadhi yao wamekua wakidai kwa abiria mtandao unasumbua na kutoa tiketi za kawaida huku wakikwepa kodi.Ally Hussein December 16, 2024 at 5:40 pm
Reply Idadi ya abiria imekuwa ndogo tofauti na tulivyozoea miaka iliyopita, sababu kuu ni kuanzwa kwa ratiba za mabasi kusafiri saa 24, na kwamba hatua hiyo imepunguza msongamano wa abiria uliokuwa ukijitokeza hasa mwishoni mwa mwaka.Adolf Locken December 16, 2024 at 5:42 pm
Reply Serikali haijatangaza kupanda kwa nauli hivyo atakayepandisha nauli hizo atakuwa amepandisha kwa maamuzi yake binafsi na si kauli ya serikali.